Pata taarifa kuu
SYRIA-MAZUNGUMZO-SIASA

Mazungumzo ya amani ya Syria yaanza Geneva, bila ujumbe wa Damascus

Umoja wa Mataifa unajaribu leo Jumanne kufufua mazungumzo ya amani ya ya Syria katika mji wa Geneva, nchini Uswisi, lakini serikali ya Damascus ambayo imeendelea kupata ushindi mkubwa wa kijeshi katika uwanja wa vita, haijatum aujumbe wake katika mazungumzo hayo.

Sergei Lavrov (kulia) akimpokea kwa mazungumzo mjumbe maalum wa U.N. kwa Syria, Staffan de Mistura wakati wa mkutano Moscow, Urusi Novemba 24, 2017.
Sergei Lavrov (kulia) akimpokea kwa mazungumzo mjumbe maalum wa U.N. kwa Syria, Staffan de Mistura wakati wa mkutano Moscow, Urusi Novemba 24, 2017. REUTERS/Sergei Karpukhin
Matangazo ya kibiashara

Mratibu wa Umoja wa Mataifa kwa Syria, Staffan de Mistura, ametangaza kwamba alikuwa amejulishwa siku ya Jumapili jioni kuahirishwa kwa ujio wa ujumbe rasmi wa serikali ya Syria katika mazungumzo ya Geneva.

"Serikali bado haijahakikishia ushiriki wake katika mazungumzo ya Geneva, lakini imesema itawasilana nasi hivi karibuni," amesema katika mkutano na Baraza la Usalama.

Pamoja na hali hiyo, Staffan de Mistura, ambaye tayari amefanya vikao 7 vya mazungumzo kati ya Wasyria mjini Geneva tangu mwaka 2016, bila mafanikio, bado ana matumani ya kupatikana kwa suluhisho katika mgogoro wa Syria. Anatarajia kuondoa hali inayotanda katika mchakato wa Geneva, kwa mara ya kwanza, kutokana na kushiriki kwa mara ya kwanza ujumbe mmoja wa upinzani wa Syria, unaowakilisha makundi yake yote, ikiwa ni pamoja na makundi yenye msimamo wa wastani, ambayo serikali ya Damascus inaona kuwa si tishio kwake.

Mnamo mwezi Septemba, De Mistura aliutaka upinzani wa Syria kuwa kuwa waangalifu kwa madai yao kwa sababu hawakushinda vita." Ikimaanisha kutodai tena kwamba suluhisho la mgogoro wa Syria ni kujiuzulu kwa rais Bashar Al Assad, ambaye serikali yake imekataa kushiriki mazungumzo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.