Pata taarifa kuu
IRAQ-IS-USALAMA

Jeshi la Iraq laurejesha kwenye himaya yake mji wa Haouidja

Vikosi vya Iraq vimetangaza leo Alhamisi kwamba wameudhibiti mji wa Haouidja, moja ya maeneo mawili ya mwisho ya kundi la Islamic State.

Wapiganaji wa Kamati za Uhamasishaji wa raia (CMP) na Jeshi la Syria karibu na mji wa Haouidja, Iraq.
Wapiganaji wa Kamati za Uhamasishaji wa raia (CMP) na Jeshi la Syria karibu na mji wa Haouidja, Iraq. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi ya majeshi yaliyozinduliwa Septemba 21 yaliendeshwa na vikosi vya serikali na wanamgambo wanaoungwa mkono na kufadhiliwa na Iran (CMP).

Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa mji wa Haouidja viunga vyake una wakazi 78,000.

Wapiganaji wa kundi la Islamic state walikua wakitumiakambi ya jeshi la anga la Rachad, kilomita thelathini kusini mwa Haouidja na kudhoibitiwa siku ya Jumatatu kama kambi ya mafunzo.

Wapiganaji wa kundi la Islamic State walidhibiti mji huo wakati wamashambulizi yao ya majira ya joto mwaka 2014, baada ya kuyatimua majeshi ya serikali.

Eneo jingine ambalo bado liko mikononi mwa kundi la Islamic Sate linapatikana magharibi mwa nchi kwenye mpaka na Syria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.