Pata taarifa kuu
ISRAEL-PALESTINA

Operesheni kabambe ya jeshi la Israel dhidi ya viwanda vya silaha

Jeshi la Israel limesema Jumanne hii kwamba limevunja viwanda saba haramu vya silaha katika Ukingo wa Magharibi, huku likikamata silaha na risasi kadhaa wakati wa operesheni iliyoelezwa kama muhimu ya aina yake kwa miaka katika ardhi ya Palestina.

Askari wa Israel wakimkagua Mpalestina katika mji wa al-Fawar, Ukingo wa Magharibi Agosti 16, 2016.
Askari wa Israel wakimkagua Mpalestina katika mji wa al-Fawar, Ukingo wa Magharibi Agosti 16, 2016. AFP
Matangazo ya kibiashara

Wakati wa operesheni hiyo iliyoendeshwa katika maeneo ya Bethlehem na Hebroni, usiku wa Jumatatu kuamkia Jumanne wik hii, askari pia walikamata mashine 22 zinazotumiwa kwa kutengeneza silaha na kukamatwa, huku wakiwakamata wafanyabiashara haramu wa silaha wawili, jeshi limesema.

Picha iliyotolewa na jeshi la Israel na polisi ya Israel inaonyesha sehemu kulikokua kukihifadhiwa bunduki ya kila aina, vifaa vya silaha na risasi.

Majeshi ya Israel wameendelea na operesheni ya kukamata silaha za moto kwa muda wa wiki moja sasa, ambapo baadhi ya silaha zilitumiwa katika wimbi la ghasia dhidi ya Israel.

Tangu mapema mwaka 2016, vikosi vya jeshi na polisi vya Israel vimegundua viwanda 29 vya silaha, vikikamata silaha za moto zaidi ya 300 na kukawamata watengenezaji na wafanyabiashara haramu wa silaha 140 katika Ukingo wa Magharibi, msemaji wa jeshi, Peter Lerner, amesema.

Kwa mujibu wa jeshi, silaha za moto zilitumika katika mashambulizi 30 dhidi ya Israel mwaka 2016.

Wapalestina 200 na Waisrael 34 wameuawa tangu Oktoba 1, 2015 kulingana na tawimu za shirika la habari la AFP.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.