Pata taarifa kuu
ISRAEL-PERES

Israel Shimon Peres alazwa hospiali kwa maradhi yasiyo ya kawaida

Rais wa zamani wa Israel na mmoja wa viongozi waliopata tuzo ya Amani ya Nobel Shimon Peres, 92, amelazwa hospitalini Jumapili baada ya maumivu ya kifua na maradhi "yasiyo ya kawaida", msemaji wake amesema.

Rais wa zamani wa Israel Shimon Peres mbele ya jengo la Bunge. Jerusalem, Julai 24, 2014.
Rais wa zamani wa Israel Shimon Peres mbele ya jengo la Bunge. Jerusalem, Julai 24, 2014. REUTERS/Ronen Zvulun
Matangazo ya kibiashara

Peres amelazwa usiku huu katika hospitali mjini Tel Aviv "chini ya uchunguzi na na vipimo mbalimbali," msemaji wake amsema katika tangazo lake.

Peres aliruhusiwa kuondoka hospitali Jumanne iliyopita baada ya kukaa siku tano na kufanyiwa upasuaji baada kufuatia tahadhari ya moyo.

Mmoja wa watetezi wa mkataba wa amani wa Oslo mwaa 1993, Shimon Peres alipata tuzo ya amani ya Nobel mwaka 1994, pamoja na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Israel Yitzhak Rabin na Rais wa zamani wa Palestina Yasser Arafat, ambao wote wawili walifariki.

Mwanasiasa wa mwisho kutoka kizazi cha waanzilishi wa taifa la Israeli kuwa hai, Bw Peres, waziri katika serikali kadhaa,na alishikilia mara kadhaa wadhifa wa Waziri Mkuu na Rais wa taifa la Israel 2007-2014.

Peres mwenye umri wa miaka 92 amebakia kuwa maarufu kupitia Kituo chake kiitwacho Peres kwa amani, ambacho kinakuza mshikamano kati ya Wayahudi na Waarabu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.