Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN- INDIA-SHAMBULIO

Afghanistan: mapigano makali kati ya jeshi na wapiganaji

Jumatatu hii, majeshi ya Afghanistan yamekua yakijaribu kuwaangamiza wapiganaji waliokimbilia katika jengo lilio karibu na ubalozi mdogo wa India katika mji wa Mazar-i-Sharif (kaskazini). Zaidi ya masaa kumi na mbili baada ya wapiganaji hawa kujaribu kudhibiti jengo hilo, bila mafanikio.

Majeshi ya usalama ya Afghanistan wakati wa operesheni dhidi ya wapiganaji Januari 4, 2016 katika mji wa Mazar-i-Sharif.
Majeshi ya usalama ya Afghanistan wakati wa operesheni dhidi ya wapiganaji Januari 4, 2016 katika mji wa Mazar-i-Sharif. FARSHAD USYAN/AFP
Matangazo ya kibiashara

Nchini India, wakati huo huo, jeshi limekua likiedesha mapigano ili kuwaondoa washambuliaji, wanaoaminika kuwa raia wa Pakistan, katika kambi ya kijeshi ya kaskazini mwa nchi hiyo.

Mashambulizi haya yanatokea siku kumi baada ya ziara ya Waziri mkuu wa India Narendra Modi nchini Afghanistan na Pakistan. Mashambulizi haya pia yanaweza kudhoofisha juhudi za maridhiano za New Delhi na Islamabad.

Hali ya usalama nchini Afghanistan, ambayo imekuwa tayari imedhoofika na mfululizo wa mashambulizi ya waasi wa Taliban, imejikuta ikidhoofika zaidi kwa shambulio la kujitoa mhanga kwa kutumia gari lilitokea Jumatatu hii asubuhi karibu na uwanja wa ndege wa mjini Kabul. "Mshambuliaji wa kujitoa mhanga pekee ameuawa", Sediq Sediqqi, msemaji wa Wizara ya mambo ya ndani ya Afghanistan amesema.

Kundi la Taliban halijakiri kuhusika na shambulio hilo, wala jaribio la washambuliaji sita la kuuteka ubalozi mdogo wa India Jumapili usiku, lakini kundi hili limekua likilenga mara kwa mara nchini Afghanistan maslahi ya New Delhi, ambayo inasaidia serikali ya Kabul.

Jumatatu hii, polisi na jeshi vya Afghanistan wamekua wakirushiana risasi na watu wenye silaha waliokimbilia katika jengo lilio karibu na ubalozi mdogo wa India.

"Operesheni ya kusafisha imeanza, mkuu wa ( mkoa wa Balkh) Atta Mohammed Noor yuko eneo hilo akisimamia operesheni hiyo", Munir Farhad, msemaji wa Bw Noor, amesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.