Pata taarifa kuu
SYRIA-MAZUNGUMZO

Syria: serikali iko "tayari" kushiriki katika mazungumzo ya amani

Serikali ya Damascus iko "tayari kushiriki" katika mazungumzo ya amani kuhusu Syria yanayotazamiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Januari mjini Geneva chini ya mwamvuli wa Umoja wa Mataifa, waziri wa mambo ya nje wa Syria, Walid Muallem, ametangaza Alhamisi hii, Desemba 24.

Waziri wa mambo ya nje wa Syria, Walid Mouallem, mbele ya wajumbe wa mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa mjini New York, Oktoba 2, 2015.
Waziri wa mambo ya nje wa Syria, Walid Mouallem, mbele ya wajumbe wa mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa mjini New York, Oktoba 2, 2015. REUTERS/Mike Segar
Matangazo ya kibiashara

Machafuko nchini Syria yamesababisha vifo vya watu 250,000 na mamilioni kukimbia makazi yao. Karibu watu milioni 4.4 wa Syria wameikimbia nchi yao, kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR).

Siku chache baada ya makubaliano kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa juu ya azimio la kupata ufumbuzi wa kisiasa kwa vita vya wenyewe kwa nchini Syria, serikali ya Damascus imetangaza kuwa iko "tayari kushiriki" katika mazungumzo ya amani.

"Serikali ya Syria iko tayari kushiriki katika mazungumzo baina ya wadau wote kutoka Syria bila kuingiliwa na mtu yeyote kutoka nje (...) wakati tutakapopokea orodha ya ujumbe kutoka upinzani", Waziri wa mambo ya nje wa Syria, Walid Muallem ametangaza.

Mkakati wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa unasisitiza mazungumzo kati ya upinzani na serikali ya Damascus, mkataba wa usitishwaji wa mapigano na kuundwa kwa serikali ya mpito katika kipindi cha miezi sita. Hatimaye, nakala hiyo inaagiza pia uchaguzi katika kipindi cha miezi kumi na nane ijayo.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi mkuu wa Umoja wa Mataifa mjini Geneva, Michael Moller, mazungumzo yajayo juu ya mustakabali wa Syria yatafanyika nchini Uswisi "mwishoni mwa mwezi Januari."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.