Pata taarifa kuu
UNSC-IS-VIKWAZO

UN yapitisha azimio kwa kuzuia fedha za kundi la IS

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekutana mjini New York kupiga kura kwa kauli moja azimio, kwa kujaribu kuzuia vyanzo vya ufadhili vya kundi la Islamic State nchini Iraq na Syria, ikiwa ni ishara muhimu kwa mapambano haya.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha kwa kauli moja azimio linalolenga kulitokomeza kundi la Islamic State, mjini New York, Desemba 17, 2015.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha kwa kauli moja azimio linalolenga kulitokomeza kundi la Islamic State, mjini New York, Desemba 17, 2015. REUTERS/Mike Segar
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huo umewashirikisha mawaziri wa fedha. Uturuki imenyooshewa kidole kwa mara nyingine tena na Urusi, inayotuhumiwa kufumbia macho kupitishwa kwa mafuta kinyume cha sheria katika ardhi yake.

Daech ni serikali, wamekumbusha mawaziri wote wa fedha ambao walikutana mjini New York. Fedha ndizo zinalipa nguvu kundi hili la Islamic State. Kwa hiyo kundi hili linahitaji fedha: linahitaji karibu Euro milioni 74,000 kwa mwezi ili kukidhi mahitaji ya watu wanaoishi katika nchi yake.

Kwa kuzuia chakula cha kundi la Islamic State kinachopatikana kupitia mafuta, jumuiya ya kimataifa inatarajia kupunguza ushawishi wake.

Shinikizo kwa Uturuki

Lakini hiyo inahitaji ushirikiano wa nchi zote na hasa wa Uturuki ambapo kunapitishwa kiasi kikubwa cha mafuta. "Uturuki kama nchi huru yenye sheria, inabdi ipambane vilivyo na biashara haramu kutoka kundi la Islamic State. Ni agizo lililotolewa kwa Uturuki kama kwa nchi nyingine jirani au nchi zilio mbali zaidi ", amesema Michel Sapin, Waziri wa Fedha wa Ufaransa.

Azimio liko wazi. linaomba serikali zote, lakini pia sekta binafsi na sekta ya benki kuzuia mitaji haramu. Nchi hizo zina miezi minne ili kuwasilisha masharti yao. Na kama hakuna kitakachofanyika, kuna uwezekano Umoja wa Mataifa ichukuwe hatua za kuziadhibu kwa kufungia mali zao kwa mfano.

Azimio Hili lilikuwa ni muhimu ili kuongeza shinikizo la kisiasa kwa kundi la kigaidi. Utekelezaji wake utakuwa muhimu kwa kupata athari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.