Pata taarifa kuu
YEMEN-UN-VITA-USALAMA

Yemen: ” Serikali iko tayari kusitisha vita ”

Serikali ya Yemen iliyokimbilia ukimbizni imeiambia Umoja wa Mataifa kuwa iko tayari kusitisha vita kwa muda ili kumaliza machafuko ya miezi mitatu yanayoendelea.

Rais Abd Rabbo Mansour Hadi, ambaye amekimbilia nchini Saudi Arabia.
Rais Abd Rabbo Mansour Hadi, ambaye amekimbilia nchini Saudi Arabia. REUTERS/Khaled Abdullah
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa serikali hiyo ya Yemen Rajeh Badi amemwambia Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon kuwa, serikali hiyo ingependa mwafaka huo kuanza kutekelezwa kwa siku chache zijazo kwa sababu za kibinadamu.

Serikali ya Yemen, imesema iko tayari kuwaachilia huru waasi wa Kihouthi wanaoshikiliwa ambao wamekuwa wakipambana na wanajeshi wa serikali.

Kiongozi wa kundi la waasi Zeifullah al-Shami amesema kuwa masharti ya serikali hayo hayakubaliki.

Wito huu wa serikali ya Yemen unakuja wakati huu kukiwa na mpango wa kuendelea kwa mazungumzo ya amani siku ya Jumapili mwishoni mwa juma hili kati ya serikali na waasi jijini Geneva.

Machafuko nchini Yemen yamekuwa yakiendelea kwa miezi mitatu na zaidi ya watu elfu tatu wamepoteza maisha kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.