Pata taarifa kuu
YEMEN-SAUDI ARABIA-HOUTHI-VITA-SIASA

Mapigano makali yarindima Aden

Aden mji wa pili wa Yemen, umeendelea kushuhudia mapigano makali kati ya wafuasi na wapinzani wa rais Abd Rabbo Hadi Mansour, baada ya siku nane ya mashambulizi ya angani yanayoendeshwa na Saudi Arabia dhidi ya waasi wa Kishia.

Watu wamesimama katika gari la kijeshi lililochomwa, Machi 29 katika mji wa Aden.
Watu wamesimama katika gari la kijeshi lililochomwa, Machi 29 katika mji wa Aden. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Takriban watu 44, ikiwa ni pamoja na raia wa kawaida 18, wameuawa katika mapigano yaliyotokea Alhamisi wiki hii katika mji wa Aden. Inaarifiwa kua huenda Ikulu ya rais katika mji wa Aden iko mikononi mwa waasi, kwa mujibu wa mashahidi na afisaa mmoja wa wizara ya ulinzi. Hata hivyo, hali bado ni tete.

Waasi wa Kishia wanasadikiwa kuwa wameiteka Ikulu ya rais mjini Aden. Kwa mujibu wa shahidi aliyehojiwa na shirika la habari la Ufaransa AFP, “ mamia ya waasi na washirika wao waliwasili Alhamisi wiki hii wakiwa katika magari yao ya kijeshi pamoja na vifaru waliingia katika Ikulu ya rais Al-Maashiq”.

Alhamisi jioni Aprili 2, afisaa mmoja wa wizara ya ulinzi alithibitisha kwamba Ikulu ya rais katika mji wa Aden iko mikononi mwa waasi, akibaini kwamba Ikulu hiyo ilikua chini ya ulinzi “ wa vikosi maalumu, vinavyomtii Ali Abdallah Saleh”, rais wa zamani aliyekabidhi madaraka mwaka 2012, baada ya mwaka mmoja wa maandamano ya raia.

Kwa mujibu wa chanzo cha kijeshi, wapiganaji wa kundi la waasi wa Kishia kutoka jamii ya Houthi, wameuawa katika mapigano hayo ya Alhamisi wiki hii. Katika mapigano hayo waliuawa pia raia wa kawaida 18 na wajumbe sita wa kamati ya iliyoundwa na raia kwa ulinzi wa mji wa Aden, kwa mujibu wa chanzo cha hospitali.

Hata hivyo hali bado ni tete katika mji wa Aden. Katika mkutano na waandishi wa habari mjini Riyadh,nchini Saudi Arabia, jenerali Ahmed Waashuri, msemaji wa muungano unaoongozwa na Saudi Arabia katika vita dhidi ya waasi, amesema kwamba hali ya usalama katika mji wa Aden " imeimarika".

" Wanamgambo wa Kishia kutoka jamii ya Houthi hawana udhibiti wa jengo lolote la serikali katika mji huo", ameongeza Ahmed Waashuri, bila hata hivyo hasa kutaja ikulu ya rais.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.