Pata taarifa kuu
ISRAELI-UCHAGUZI-SIASA

Siku ya uchaguzi Israeli: raia waitikia kwa wingi

Karibu Waisraeli milioni 6 wamekua wakisubiriwa Jumanne wiki hii katika vituo vya kupigia kura nchi nzima ili kuwachagua wabunge 120, na kuamua kama bado wanamtaka tena Benjamin Netanyahu madarakani au la.

Raia aliyeshiriki uchaguzi akiingiza kadi ya uchaguzi katika sanduku la kura, katika mji wa Ramat Gan, karibu na Tel-Aviv, MAchi 17 mwaka 2015.
Raia aliyeshiriki uchaguzi akiingiza kadi ya uchaguzi katika sanduku la kura, katika mji wa Ramat Gan, karibu na Tel-Aviv, MAchi 17 mwaka 2015. RFI
Matangazo ya kibiashara

Waziri mkuu anaye maliza muda wake anakabiliwa na wakati mgumu, kwani chama chake cha mrengo wa kulia, Likud, kimeachwa mbali kabisa katika uchaguzi, huku chama cha mrengo wa kati-kushoto kikiongoza.

Kuelekea uchaguzi wa leo, kura za maoni zimekuwa zikimpa nafasi kubwa kiongozi wa upinzani bwana Herzog lakini wadadisi wa mambo wanasema huenda chama cha Netanyahu kikawa na ushawishi wa kuomba muungano wa vyama vingine baada ya uchaguzi wa leo.

Saa nne saa za Israeli, kiwango cha waliokua wameshashiriki uchaguzi kilikua asilimia 13.7. Baadae mchana, kwa mujibu wa Haaretz, ushiriki ulikua kwenye kiwango cha asilimia 26.5, na kisha asilimia 36.7 saa nane. Orodha ya chama cha mrengo wa kati-kushoto ilikua ikiendelea kupanda dhidi ya chama cha Likud cha waziri mkuu anaye maliza muda wake Benjamin Netanyahu.

Kwa mujibu wa waandishi wa RFI, waliotumwa katika maeneo mbalimbali nchini Israeli, Michel Paul, Murielle Paradon na Nicolas Falez, Muungano wa Kizayuni umewakilishwa na watu wawili ambo ni mwanaume na mawanamke. Mwanaume ni Yitzhak Herzog, akijulikana kwa jina la Bouji. Yitzhak Herzog, mwenye umri wa miaka 54, ni kiongozi wa chama cha Lebour, akiwa pia mtoto wa rais wa taifa la Israeli.

Mwanamke ni Tzipi Livni, mwenye umri wa miaka 56. Aliwahi kuwa waziri wa mambo ya nje, huku akibaini kwamba kuundwa kwa taifa la Israeli kutapelekea Israeli inakua taifa huru na lenye misingi ya kidemokrasia.

Hata hivyo Waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu ameapa kuwa hakutakua na taifa huru la Palestina kama atakua bado madarakani.

Yitzhak Herzog na Tzipi Livni walibaini Jumatatu wiki hii kwamba kama wanashinda watakua wakibadilishana kwenye wadhifa wa waziri mkuu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.