Pata taarifa kuu
SAUDIA ARABIA-KIFO-UFALME-SIASA

Mfalme Abdallah afariki

Mfalme Abdallah wa Saudi Arabia amefariki leo Ijumaa Janauri 23, familia ya mfalme imefahamisha katika tangazo ililolitoa mapema asubuhi.

Mfalme Abdullah bin Abdulaziz Al Saud wa Saudi Arabia, akiwa katika Kasri lake mjini Riyadh, Septemba 11 mwaka 2014.
Mfalme Abdullah bin Abdulaziz Al Saud wa Saudi Arabia, akiwa katika Kasri lake mjini Riyadh, Septemba 11 mwaka 2014. AFP PHOTO/POOL/BRENDAN SMIALOWSKI
Matangazo ya kibiashara

Mfalme Abdallah, mwenye umri wa miaka 90, alilazwa hospitalini mjini Riyadh, Desemba mwaka jana kutokana na maradhi ya nimonia. Mwanamfalme Salman, mwenye umri wa miaka 77, ndiye anarithi kiti cha mfalme. Moqren, ndugu wa Abdallah, ameteuliwa kuwa mrithi wa mwanamfalme Salman.

 " Mheshimiwa Salman bin Abdul-Aziz Al Saoud na familia ya Abdul-Aziz Al Saoud pamoja na taifa nzima tunaomboleza kifo cha mlinzi wa Misikiti miwli Mitakatifu, mfalme Abdallah bin Abdulaziz, ambaye amefariki saa saba usiku wa kuamkia leo Ijumaa", limesema tangazo hilo.

Akikabidhiwa rasmi mamlaka ya kukalia kiti cha ufalme mwaka 2005 baada ya kifo cha ndugu yake Fahd, mfalme Abdullah alishikilia madaraka ya uongozi wa nchi ya Saudia Arabia kwa kipindi cha miaka mingi kutokana na kudhohofika kwa afya ya Fahd, ambaye alimteua kuchukua madaraka ya uongozi wa nchi kwa muda, tangu mwaka 1996.

Alipokuwa mwanamfalme mrithi, Abdallah alikuwa mmoja wa wabunifu maarufu wa makubaliano ya Taif ambayo yalipelekea kumalizika kwa vita nchini Lebanon mwishoni mwa miaka ya 1980. Baada ya kukabidhiwa kwa muda madaraka ya uongozi wa nchi, mfalme Abdallah alijihusisha na muungano wa nchi yake na adui yake mkubwa Iran, wakati Mohammad Khatami alikua mmoja wa viongozi vigogo wa Tehran.

Historia inaarifu kuwa mfalme Abdallah ndiye aliyeanzisha mazungumzo kati ya dini mablimbali na Vatican. Hata hivyo, katika suala la haki za binadamu, wanawake bado wameendelea kupigwa marufu ya kusafiri peke yao au kuendesha gari. Na adhabu ya kifo bado inathaminiwa nchini Saudia Arabia.

Rais wa Ufaransa Francois Hollande ametoa salamu za rambirambi kwa familia ya mfalme, huku akikaribisha "kumbukumbu ya mfalme huyo ambaye kazi yake ina maana kubwa kwa historia ya nchi yake, na mchakato wa amani ya kudumu katika Mashariki ya Kati bado ni miongoni mwa kazi ambazo zitakumbukwa mno alizofanya mfalme Abdallah", Ikulu ya rais Ufaransa imesema katika tangazo lake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.