Pata taarifa kuu
SYRIA-MAREKANI-IS-Mashambulizi-Usalama

Syria: muungano wa waasi waahitaji silaha dhidi ya Bashar na IS

Muungano wa waasi nchini Syria umeomba upewe silaha ili kuuondoa utawala wa Bashara Al Assad, wakati Marekani ikianzisha mashambulizi kwa mara ya kwanza nchini Syria dhidi ya wapiganaji wa Dola la Kiislam katika mji wa Raqqa.

Wapiganaji wa muungano wa waasi nchini Syria katika mji wa Allepo.
Wapiganaji wa muungano wa waasi nchini Syria katika mji wa Allepo. REUTERS/Hosam Katan
Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi hayo yaliombwa kwa muda mrefu na upinzani wa Syria, ambao wawakilishi wake wamejielekeza mjini New York kukutana na viongozi wa kisiasa wakati huu ambapo unafanyika mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Mashambulizi hayo ya Marekani yamepelekea Muungano wa waasi wenye msimamo wa wastani nchini Syria kupata nguvu baada ya kuoneka hivi karibuni kudhohofika wakidai kwamba ni kutokana na ukosefu wa silaha.

Kiongozi wa upinzani nchini Syria Hadi Al-Bhra , ambaye amejielekeza mjini New York, amesema ana imanai kuwa ahadi za Marekani za kuwapa silaha zitatekelezwa, na kupelekea waasi wanaendesha vita vya chini hadi kuung'oa utawala wa Bashar Al Assad.

Hadi Al Bahri amependekeza kwamba mashambulizi hayo yaendeshwe pia dhidi ya majeshi ya Bashar Al Assad, ambaye, muungano huo unadai kwamba ndiye chanzo cha mgogoro nchini Syria.

Upinzani huo wa Syria umeomba kutengwe eneo la mashambulizi ya anga ili ngome wapiganaji wa Muungano wa waasi zisishambuliwe katika eneo la Allepo na kuwashirikisha katika uendeshaji wa mashambulizi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.