Pata taarifa kuu
PALESTUNA-ISRAELI-HAMAS-Usalama

Palestina: makubaliano ya kuongeza muda wa kusitisha mapigano yakabiliwa na kizungumkuti

Usuluhishi wa mgogoro wa Israeli na Palestina nchini Misri umetangaza siku ya Jumatano makubaliano yaliyofikiwa ya kuongeza kwa muda wa siku tano ya kusitisha mapigano kati ya Israel na Hamas licha ya Israeli kuanzisha upya mashambulizi ya anga kujibu mashambulizi ya makombora ya Hamas.

Watoto wa kipalestina katika mji wa Khan Younès, ambao unaendelea kushambuliwa na jeshi la Israeli katika ukanda wa Gaza.
Watoto wa kipalestina katika mji wa Khan Younès, ambao unaendelea kushambuliwa na jeshi la Israeli katika ukanda wa Gaza. REUTERS/Ibraheem Abu Mustafa
Matangazo ya kibiashara

Wakati muda wa kusitisha mapigano ukiongezwa kwa siku tano, duru kutoka Wizara ya mambo ya ndani ya Palestina, ndege za kivita za Israel zimefanya mashambulizi katika usiku wa Jumatano kuamkia Alhamisi wiki hii kwenye ukanda wa Gaza saa chache baada ya kutangazwa kwa muda mwingine wa kusitisha vita, huku jeshi la Israeli likidai kujibu makombora sita yaliyorushwa na Hamas.

Machafuko hayo yanakuja wakati pande zote mbili katika mazungumzo yanayoendelea nchini Misri wakikubaliana upanuzi wa muda wa kusitisha vita ili kuruhusu majadiliano zaidi baada ya mgogoro uliodumu kwa zaidi ya mwezi moja na kusababisha vifo vya zaidi ya raia elfu mbili wa kipalestina huku Israel ikipoteza wanajeshi 65 na raia wa tatu.

Muda huo wa kusitisha vita utafikia mwisho wake siku ya jumanne wakati mazungumzo yakiendelea chini ya usimamizi wa Usalama wa taifa la Misri ambapo suala la msingi na gumu kufikia ufumbuzi wake ni ombi la Hamas kwa Israel kuondowa vizuizi vilivyowekwa na Israel tangu 2007.

Mapema siku ya jumatano, watu sita wameuawa na mlipuko wa kombora la Israeli miongoni mwao Simone Camilli mwenye umri wa miaka 35 na mpigapicha wa shirika la habari la “Associated Press” ambaye ndiye mwandishi wa habari wa kigeni wa kwanza kuuawa katika vita hivyo vilivyo dumu zaidi ya mwezi mmoja sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.