Pata taarifa kuu
ISREALI-PALESTINA-HAMAS-Mapigano

Gaza : shule zinazodhaminiwa na UN zalengwa kwa mashambulizi

eshi la israeli linaendelea na mashambulizi kwa siku ya 17 alhamisi wiki hii katika ukanda wa Gaza dhidi ya kundi la Hamas. Zaidi ya wapalestina 700 wameuawa tangu mashambulizi ya Israeli yaanze katika ukanda wa Gaza, huku idadi ya wanajeshi wa Israeli waliyouawa ikiwa imefikia 32.

Wakimbizi wa kipalestina wakiomba hifadhi kwenye shule zinzodhaminiwa na Umoja wa Mataifa, Julai 21 mwaka 2014.
Wakimbizi wa kipalestina wakiomba hifadhi kwenye shule zinzodhaminiwa na Umoja wa Mataifa, Julai 21 mwaka 2014. REUTERS/Finbarr O'Reilly
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, wapalestina 100.000 wameyahama makaazi yao kufutia mashambulizi hayo ya Israeli, huku baadhi wakiwa wamepewa hifadhi kwenye shule zinazodhaminiwa na Umoja wa Mataifa, bila hata hivo kuwa na ulinzi wa kutosha.

Wapalestina wakiwasili kwenye shule inayodhaminiwa na UN, badaa ya kuyakimbia mashambulizi ya jeshi la Israeli katika eneo la Rafah, kusini mwa Gaza..
Wapalestina wakiwasili kwenye shule inayodhaminiwa na UN, badaa ya kuyakimbia mashambulizi ya jeshi la Israeli katika eneo la Rafah, kusini mwa Gaza.. REUTERS/Ibraheem Abu Mustafa

Kwa sasa shule hizo zimeanza kulengwa kwa mashambulizi, baada ya kuonekana kwamba kuna watu wanaorusha makombora wakijificha kwenye shule hizo.

Wakati huo huo, waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry, anaendelea na jitihada zake katika za kukutanisha Iraeli na Hamas kwa lengo la kusitisha mapigano. Kerry anatazamiwa kujielekeza kwa mara nyingine nchini Misri. Misri imekua ikishawishi Israeli na Hamas kuketi kwenye meza ya Mazungumzo ili kukomesha uhasama baina yao.

Awali Misri ilipendekeza pandehizo mbili kusitisha mapigano kwa minajili ya kuruhusu mashirika ya kihisani kufikishia chakula walengwa.

Hata hivo mapigano hayo yameanza kuleta athari katika sekta ya biashara nchini Israeli. Zaidi ya mashirika ya usafiri kumi yamesitisha safari za ndege nchini Israeli. Marekani ambaye ni mshirika wa karibu wa Israeli, imefuta hatua hiyo ya kusitisha kwa safari za ndege nchini Israeli.

Shirika la usafiri wa ndege la Marekani (FAA) limeruhusu ndege zake kusafiri nchini Israeli, lakini limeonya kuwa hali ya usalama bado ni tete.

Hayo yakijiri, rais wa Israeli Reuven Rivlin anamrithi rasmi alhamisi wiki hii Shimon Peres.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.