Pata taarifa kuu
SYRIA-LEBANONI

Hezbollah yajiapiza kuwaangamiza wafuasi wa Rais Bashar Al Assad wa Syria

Kiongozi wa kundi la Hezbollah la nchini Lebanon linalounga mkono serikali ya Rais Bashar Al Assad wa Syria, Hassan Nasrallah amewaahidi wafuasi wake kuwa ni lazima waibuke na ushindi katika vita dhidi ya wale wanaompinga Rais Assad.

REUTERS/Sharif Karim
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi huyo amesema hawatokubali kushindwa katika vita hivyo kwani hatua hiyo itawapa madaraka wapinzani wa Assad ambao amewataja kama vibaraka wa Marekani na Israel.

Kauli hiyo inakuja wakati mapigano makali yakiendelea kushuhudiwa kati ya vikosi tiifu kwa Rais Assad na waasi ambao bado hawajaonyesha nia ya kushiriki katika mazungumzo ya kutafuta suluhu ya mgogoro wao mjini Geneva.

Mapigano ya siku ya jumamosi katika mji wa Qusayr yamesababisha vifo vya watu zaidi ya 40 idadi ambayo imetajwa ni kubwa kutokea katika kipindi cha siku moja miongoni mwa siku saba mfululizo za mapigano zilizoshuhudiwa katika juma hili.

Katika siku tatu za mkutano wa wapinzani wa Syria mjini Istanbul bado jitihada za kushinikiza mazungumzo hazijazaa matunda kwani bado wameendelea na msimamo wao wa kutotaka mazungumzo mpaka pale Rais Assad atakapoondoka madarakani.

Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa UN, machafuko ya Syria yamesababisha vifo vya watu zaidi ya elfu 94,000 tangu yaliposhika kasi mwezi machi mwaka 2011.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.