Pata taarifa kuu
Afghanistani

Shambulizi la bomu laua 14 Afghanistan

Shambulizi la bomu lililokuwa limetegwa ndani ya gari limesababisha vifo vya watu 14 wakiwemo wanajeshi sita wa umoja wa kujihami wa nchi za Magharibi NATO mjini Kabul nchini Afghanistan.

Raia wakishuhudia madhara ya bomu
Raia wakishuhudia madhara ya bomu interaksyon.com
Matangazo ya kibiashara

Bomu hilo lilienga msafara wa majeshi ya NATO na miongoni mwa waliopoteza maisha ni pamoja na watoto wawili na kusababisha watu wengine 37 kujeruhiwa.

Kundi la kigaidi la Hezbi-i Islami ambalo linashirikiana kwa karibu na lile la Taliban limekiri kutekeleza shambulizi hilo.

Hili ndilo shambulizi baya zaidi kuwahi kutokea mjini Kabul katika siku za hivi karibuni baada ya shambulizi lingine kutokea mwezi wa tatu mwaka huu na kusababisha vifo vya watu tisa wakati wa ziara ya waziri wa ulinzi wa Marekani Chuck Hagel nchini humo.

Majeshi ya Nato zaidi ya laki moja ambayo yapo nchini Afghanistan kupambana namkundi ya kigaidi kama Taliban, yanatarajia kumaliza operesheni yake kufikia mwishoni mwa mwaka ujao, baada ya operesheni hiyo kudumu kwa miaka 11.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.