Pata taarifa kuu
Syria

Mazungumzo kati ya Upinzani na Serikali ya Syria kufanyika siku ya Alhamisi

Mazungumzo baina ya wajumbe kutoka kwa mataifa yanayojiita marafiki wa Syria yanatarajiwa kufanyika kesho Alhamisi mjini Roma nchini Italia. 

Rais wa Syria, Bashar Al Assad
Rais wa Syria, Bashar Al Assad AFP PHOTO/SYRIAN TV
Matangazo ya kibiashara

Mazungumo hayo yanalenga kumaliza machafuko nchini humo ambayo yanaendelea kwa mwaka wa pili sasa na tayari upinzani nchini Syria umekubali kushiriki katika mazungunmzo hayo.

Awali juhudi za mazungumzo kuhusu Syria hazikuzaa matunda kwa kile kinachoelezwa na wachambuzi wa siasa kuwa ni kutokana na kutowezekana kwa upinzani na serikali nchini Syria kukaa katika meza moja ya mazungumzo.

Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov alitoa wito kwa Viongozi wa upinzani nchini Syria kuanzisha mazungumzo na Utawala ili kukomesha mauaji.

Wakati juhudi za kidiplomasia za kumaliza mzozo wa Syria zikipamba moto, mapigano yameibuka katika mji wa pili kwa ukubwa Aleppo.

Umoja wa Mataifa umesema kuwa Watu 150,000 wamekimbia mapigano Mwezi huu.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.