Pata taarifa kuu
Pakistani

Watu 115 wauawa kwa Shambulio la Bomu nchini Pakistani

Takriban Watu 115 wameuawa kwa shambulio la Bomu Nchini Pakistan hali iliyosababisha uwepo wa wasiwasi wa kuwepo kwa Machafuko wakati nchi hiyo inapoelekea katika Uchaguzi Mkuu.

Rais wa Pakistani, Asif Ali Zardari
Rais wa Pakistani, Asif Ali Zardari
Matangazo ya kibiashara

Watu 82 waliuawa na wengine 121 kujeruhiwa kwa mabomu mawili ya kujitoa Muhanga yaliyolenga Kundi kubwa la Watu katika Kilabu kimoja mjini Queta, katika eneo linalikaliwa na Waislamu wengi wa Madhehebu ya kishia wa jamii ndogo ya Hazara.
 

Kundi la Kiislam lenye msimamo Mkali wa Madhehebu ya Sunni la Lashkar-e- Jhangvi limedai kuhusika na shambulio hilo linaloelezwa kuwa kubwa zaidi kufanyika dhidi ya Washia.
 

Shambulio hilo la hivi karibuni linaelezwa kuwa baya zaidi tangu yalipotokea mashambulizi mawili ya kujitoa Muhanga na kusababisha watu 98 kupoteza maisha.
 

Serikali ya Pakistan imetangaza siku tatu za Maombolezo Mjini Baluchistan na Fidia ya dola za kimarekani 20,560 kwa Familia za Maafisa wa Polisi waliouawa na rupia milioni moja kwa Familia za Raia waliouawa.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.