Pata taarifa kuu
PAKISTAN

Maiti ishirini na moja za Polisi waliotekwa zapatikana nchini Pakistan

Maiti za polisi ishirini na moja wanaosadikiwa kuwa walitekwa kwa muda wa siku mbili na wapiganaji wa Taliban zimepatikana katika eneo la Jabai kaskazini magharibi mwa Pakistan mapema leo jumapili asubuhi, maofisa wa serikali wamethibitisha kupatikana kwa miili hiyo.

REUTERS/Mohammad Ismail
Matangazo ya kibiashara

Polisi mmoja amekutwa katika eneo hilo akiwa katika hali mbaya baada ya vyombo vya dola kupata taarifa toka kwa polisi mmoja ambaye alifanikiwa kuwatoroka wauaji akiwa hai.

Polisi ishirini na watatu walipotea baada ya shambulizi la alhamisi katika vituo viwili mjini Peshawar ambapo polisi wawili waliuawa papo hapo na wengine kujeruhiwa.

Kundi la Taliban limekuwa likifanya mashambulizi kwa takribani muongo mmoja kukabiliana na serikali ya Pakistan na majeshi ya kigeni yaliyopo nchini humo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.