Pata taarifa kuu
Lebanon

Wawili wauwawa, sita wajeruhiwa katika machafuko mapya nchini Syria

Raia wawili wa Lebanon wameuwawa na wengine sita wamejeruhiwa katika mji wa Kaskazini mwa Lebanon wa Tripoli , baada ya mapigano ya usiku wa manane jana Jumamosi huku kukiwa na mapigano ya madhehebu ya kidini yanayohusishwa na vita katika nchi jirani ya Syria, afisa usalama amesema. 

Machafuko yashika kasi huko Syria
Machafuko yashika kasi huko Syria wrnewz.com
Matangazo ya kibiashara

Mapigano hayo ya bunduki na roketi yaliibuka kati ya wakazi wa wilaya maskini ya Bab al- Tebbaneh na Jabal Mohsen, ambao wanaabudu katika madhehebu ya Sunni dhidi ya Alawites ambao ni jamii ya kidini ya rais wa Syria Bashar al-Assad.

Mauaji ya watu hao wawili wa Jabal Mohsen yalivunja utulivu ambao umekuwepo tangu Ijumaa asubuhi, wakati jeshi lilipopeleka askari katika maeneo ya eneo hilo la mji wa bandari.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.