Pata taarifa kuu
Lebanon

Lebanoni yatolewa wito kuunda Serikali mpya ya Muungano

Shinikizo zaidi kutoka kwa mataifa ya Magharibi zimeendelea kutolewa kwa Lebanon kubuni serikali mpya ya muungano baada ya shambulizi la bomu mjini beirut wiki iliyopita na kusababisha kuuliwa kwa afisa wa ujasusi nchini humo Wissam al-Hassan.

Afisa wa Ujasusi wa Lebanoni aliyeuawa kwa mashambulizi yanayoelezwa kutekelezwa na Syria
Afisa wa Ujasusi wa Lebanoni aliyeuawa kwa mashambulizi yanayoelezwa kutekelezwa na Syria
Matangazo ya kibiashara

Marekani imesema kuwa inaunga mkono juhudi hizo za uundaji wa serikali mpya nchini humo hasa baad aya Lebanon kuhusishwa na machjafuko nchini Syria ambayo yanaelezwa kuwa huenda yakasambaa hadi katka mataifa jirani.

Nalo shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi limesitisha kwa muda zoezi la kuwasajili wakimbizi kutoka nchini Syria wanaokimbilia Lebanon kwa hofu ya usalama nchini humo.

Katika hatua nyingine, Marekani na Umoja wa Ulaya umeeleza kusikitishwa kwake na hali ya mpasuko wa kisiasa nchini Lebanon, ambapo Upinzani umetaka Waziri Mkuu wa nchi hiyo kujiuzulu baada ya Shambulio kufanyika dhidi ya nchi hiyo ambapo Syria inashutumiwa kuhusika.

Lebanon pia imeathiriwa kutokana na wimbi kubwa la Wakimbizi kutoka Syria, huku Shirika la Umoja wa Mataifa likisema kuwa idadi yao ni zaidi ya 100,000.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.