Pata taarifa kuu
Syria

Lakhdar Brahimi aziomba pande zinazohasimiana nchini Syria kuacha Mapambano

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia Mgogoro wa Syria, Lakhadar Brahimi ametoa wito kwa pande mbili zinazopambana nchini Syria kuacha mapigano wakati huu wanapoelekea katika sikukuu ya Eid al Haj baada ya kufanya mazungumzo na Rais wa nchi hiyo, Bashar Al Assad.

Lakhdar Brahimi akizungumza na Rais wa Syria, Bashar Al Assad
Lakhdar Brahimi akizungumza na Rais wa Syria, Bashar Al Assad REUTERS/Sana
Matangazo ya kibiashara

Wito huo umekuja wakati ambapo maelfu ya Watu wameandamana kupinga utawala wa Syria wakati wa Mazishi ya Mkuu wa maswala ya intelijensia wa Lebanon, aliyeuawa kwa Bomu,mauaji yanayoelezwa kutekelezwa na Vikosi vya Syria.
Β 

Shambulio hilo limetokea wakati ambapo Brahimi akizitaka pande mbili kwa pamoja kuweka silaha chini kwa ajili ya kuheshimu siku hiyo takatifu.
Β 

Ingawa amesisitiza kuwa wito huo wa kuweka silaha chini ni wa hiari, kwa pamoja Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon na Mkuu wa Jumuia ya Nchi za Kiarabu, Nabil al Arabi wameunga mkono Jitihada hizo.
Β 

Brahimi amesema amewasiliana na Viongozi wa kisiasa wa upinzani ndani na nje ya Syria na Makundi ya Watu wenye silaha nchini humo, na ameahidi kurejea tana Syria baada ya sikuu ya Eid kuendelea na Mchakato wa kurejesha amani nchini humo.
Β 

Assad, wakati wa mkutano wake na Brahimi, amesema kuwa yuko tayari kwa juhudi zozote zenye nia njema ya kutafuta suluhu la kisiasa kwa kulenga kuheshimu mamlaka ya Syria bila kuingiliwa na mataifa ya nje.
Β 

Brahimi pia alikutana na Mabalozi wa Urusi na China, nchi zilizozuia Maazimio ya UN kuchukua hatua dhidi ya Syria ndani ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Β 

Β 

Β 

Β 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.