Pata taarifa kuu
SYRIA-LEBANON

Raisi wa syria alaumiwa kwa shambulizi la Beirut

Shambulizi la bomu lililotekelezwa kwenye gari na kuua watu 8 huko Beirut akiwemo afisa wa usalama wa nchini Lebanon limehusishwa na mapambano ya kushambulia kambi ya Damascus na kusababisha upinzani kuitaka serikali ya Syria kujiondoa madarakani.

Moja kati ya vifaa vya kijeshi vinavyomilikiwa na serikali ya Sryia vinavyotumika katika mashambulizi
Moja kati ya vifaa vya kijeshi vinavyomilikiwa na serikali ya Sryia vinavyotumika katika mashambulizi REUTERS/via Reuters TV
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa mawasiliano Walid Dauk amesema kuwa mashambulizi yaliyofanyika katika eneo Ashrafieh limesababisha takribani watu 86 kujeruhiwa.

Tayari viongozi wawili wa kisiasa sambamba na kundi kuu la upinzani huko Lebanon wamemlaumu raisi wa Syria Bashar al Assad kufuati shambulizi hilo ambalo limesababisha lawama za kimataifa.

Miongoni mwa waliopoteza maisha alikuwepo mkuu wa majeshi ya usalama wa taifa hilo generali Wissam al Hassan,ambaye kifo chake kinaweka kumbukumbu nyingine ya mauaji tangu iliyotokea mwaka 2005 ambapo waziri mkuu wa zamani Rafiq Hariri aliuawa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.