Pata taarifa kuu
IRAN-UAE

Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za kiarabu za ghuba kukutana mjini Doha kujadili mgogoro wa kisiwa kati ya Iran na UAE

Mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa nchi za Ghuba wanatarajiwa kukutana mjini Doha nchini Qatari kwaajili ya mkutano utakao jadili mgogoro wa kisiwa kimoja ambacho kinagombewa na nchi ya Iran na Umoja wa Falme za kiarabu UAE. 

Rais wa Iran, Mahamoud Ahmedneijad
Rais wa Iran, Mahamoud Ahmedneijad Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huo ambao ulikuwa ufanyike Abudhabi sasa umethibitishwa kuwa utafanyika mjini Doha ambapo mawaziri hao watajadili namna ya kutatua mzozo ambao umeanza kujitokeza.

Juma lililopita Abu Dhabi ilimuita nyumbani balozi wake mjini Tehran kama hatua moa wapo ya kuonyesha kupinga zaira ambayo imefanywa hivi karibuni na rais wa Iran Mahamud Ahmedneijad.

Kisiwa cha Abu Musa kimekuwa kikigombewa na nchi hizo mbili ambapo Umoja wa Mataifa UN unakitambua kisiwa hicho kama miliki ya UAE na sio Iran jambo ambalo Iran imekuwa ikipinga.

Mbali na kisiwa hicho nchi hizo mbili pia zinagombea visiwa vingine viwili kusini mwa Ghuba ya nchi hizo jambo ambalo linazua hofu ya kuzuka vita kati ya nchi hizo mbili.

Kwa mujibu wa maofisa wanaosimamia mkutano huo wamesema kuwa, viongozi wa pande mbiloi wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huo ambao utajaribu kuja na suluhisho la mgogoro huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.