Pata taarifa kuu
SYRIA-DAMASCUS

Maelfu waendelea kukimbia mapigano nchini Syria

Ikiwa ni siku moja tu imebaki kabla ya ujumbe maalumu wa Umoja wa mataifa unaoongozwa na aliyekuwa katibu mkuu wa umoja huo Koffi Annan kuwasili nchini Syria kwa mazungumzo, maelfu ya waanchi wameendelea kuikimbia nchi hiyo kuhofia maisha yao. 

Wanajeshi wa jeshi huru la Syria wakiwa na silaha tayari kukabiliana na majeshi ya serikali
Wanajeshi wa jeshi huru la Syria wakiwa na silaha tayari kukabiliana na majeshi ya serikali Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa taarifa ya tume ya Umoja wa Mataifa inayojishughulisha na utoaji misaada imesema kuwa maelfu ya wananchi wameendelea kukimbilia nchi jirani za Lebanon na Uturuki kukimbia mapigano yanayoendelea nchini humo.

Shirika la msalama mwekundu nchini Syria limesema kuwa zaidi ya wananchi elfu mbili wamewasili kwenye maeneo ya mpakani mwa nchi hizo na Syria wakiomba kupatiwa hifadhi kufuatia mapgano yanyoendelea kati ya vikosi vya serikali jeshi huru la Syria.

Mpaka sasa zaidi ya watu elfu saba na mia tano wanahofiwa kupoteza maisha kutokana na machafuko hayo ambayo sasa yametimiza mwaka huku wanaharakati wakiendelea kusisitiza kujiuzulu kwa serikali ya rais Asad.

Machafuko hayo yanaongezeka wakati ambapo katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Koffi Annan na ujumbe wake wanatarajiwa kuwasili nchini humo hapo kesho na kutarajiwa kukutana kwa mazungumzo na rais Asad.

Kiongozi huyo na ujumbe wake wamepanga kufanya mazungumzo na serikali na baadae viongozi wa upinzani ambao wamekuwa wakifanya harakati zao kwenye mji wa Homs ambako ndiko iliko ngome kubwa ya jeshi huru la Syria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.