Pata taarifa kuu
YEMEN

Zaidi ya wanajeshi 70 wa Yemen na wanamgambo 25 wa Al-Qaeda wamekufa kwenye mapigano kusini mwa nchi hiyo

Kumefanywa shambulio la kushtukiza kusini mwa nchi ya Yemen kwenye miji ya Zinjibar na Abyan ambapo zaidi ya wanajeshi 70 na wanamgambo 25 wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa kundi la Al-Qaeda wamekufa.

Baadhi ya wananchi wa Yemen ambao ni viongozi wa makabila wanaodaiwa kushirikiana na wanamgambo wa Al-Qaeda kusini mwa nchi hiyo
Baadhi ya wananchi wa Yemen ambao ni viongozi wa makabila wanaodaiwa kushirikiana na wanamgambo wa Al-Qaeda kusini mwa nchi hiyo Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa taarifa za polisi kwenye miji hiyo zinasema kuwa idadi ya wanajeshi hao na wanagambo waliokufa wakati wa mapigano huenda ikaongezeka kutokana na wengi wao kujeruhiwa vibaya wakati wa makabiliano ya risasi na mabomu.

Shambulio hilo limefanywa siku ya jumapili ambapo kundi la wanamgambo wa Al-Qaeda walivamia kambi za jeshi kwenye miji hiyo na kufanya mashambulizi ya kushtukiza yaliyosababisha vifo hivyo.

Kwenye taarifa ya jeshi la nchi hiyo imesema kuwa, wanajeshi kwa kushirikiana na polisi walifanikiwa kuzima mashambulizi hayo na kwamba wameimarisha ulinzi kwenye maeneo ya miji hiyo kulinda wananchi.

Wapiganaji wa Al-Qaeda wamekuwa wakifanya mashambulizi yakushtukiza dhidi ya vikosi vya serikali kwenye miji ya kusini mwa nchi hiyo ambapo tukio la hapo jana wanamgambo hao walikuwa wakijaribu kuteka kituo cha polisi cha Kudi.

Serikali ya Yemen imeahidi kukabiliana na wapiganaji hao ambao wamekuwa wakitekeleza shughuli zao kusini mwa nchi hiyo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.