Pata taarifa kuu
IRAQ

Watu zaidi ya 27 wauwa kwenye mashambulizi katika mji wa Haditha nchini Iraq

Mtu mmoja mwenye silaha ameshambulia kituo cha polisi cha ukaguzi magharibi mwa nchi ya Iraq kwenye mji wa Haditha na kuua watu zaidi ya ishirini na saba.

Ramani ya nchi ya Iraq
Ramani ya nchi ya Iraq Online
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa jeshi la polisi kwenye mji huo Luteni Kanali Owaid amesema kuwa watu hao ambao wanadaiwa kuwa ni wafuasi wa kundi la Al-Qaeda walifanya mashambulizi kwenye vituo vya ukaguzi na kuua watu ambapo amethibitisha kuuawa kwa askari watano.

Mbali na wapiganaji hao kutekeleza mashambulizi hayo kwenye vituo vya polisi walianza kwa kuwakamata wakuu wa vituo kadhaa vya polisi na kisha kuwapeleka hadharani na kuwafyatulia risasi.

Msemaji huo ameongeza kuwa mashambulizi hayo yamefanyika kwa muda tofauti ingawa yote kwa pamoja yanaonekana kuwa yalikuwa yamepangwa kikamilifu kutokana na kupisha muda mchache.

Wananchi kwenye mji huo wamewekwa kwenye hali ya tahadhari huku polisi wakitoa wito kwa wananchi kurikiana kuwabaini watu ambao wanahisi kuwa wanshirikiana na wanamgambo wa Al-Qaeda kutekeleza mashambulizi hayo.

Toka kuondoka kwa vikosi vya Marekani na washirika wake nchini humo mashambuzli dhidi ya raia yamekuwa yakiongezeka na kuzua hofu kuhusu uimara wa vikosi vya nchi hiyo kuweza kudhibiti mashambulizi kama hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.