Pata taarifa kuu
Pakistan

Pakistani yasema itasaidia juhudi za amani nchini Afghanistani.

Pakistani imesema kuwa itasaidia katika juhudi zote za kuimarisha maridhiano nchini Afghanistan wakati huu ambapo waziri mkuu Yousuf Raza Gilan anataraji kuzuru Qatar hapo kesho kwa ajili ya mazungumzo ya kutafuta amani. 

Waziri mkuu wa Pakistan Yousuf Raza Gilani
Waziri mkuu wa Pakistan Yousuf Raza Gilani Reuters/Mian Khursheed
Matangazo ya kibiashara

Ziara ya waziri Gilan inakuja ikiwa ni mwezi mmoja baada ya kundi la Taliban kusema kuwa linapanga kuanzisha ofisi ya kisiasa huko Qatar wakati wa hatua za kuelekea mazungumzo ya amani na nchi ya Marekani.

Waziri wa Nje wa Pakistan Hina Rabbani Khar wakati wa ziara yake mjini Kabul wiki iliyopita alikataa madai kuwa nchi yake imekuwa ikiliunga mkono kwa siri kundi la Taliban nchini Afghanistan.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.