Pata taarifa kuu
Pakistan

waziri mkuu wa Pakistan,Yousef Raza Gilani akubali kufika mahakamani.

Waziri Mkuu wa Pakistan Yousef Raza Gilani amekubali kufika Mahakamani siku ya alhamisi kujibu tuhuma za yeye kushindwa kumfungulia mashtaka Rais Asif Ali Zardari na viongozi wengine wanaotajwa kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Rais wa Pakistan Asif Ali Zardari
Rais wa Pakistan Asif Ali Zardari REUTERS/Murad Sezer
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huo unakuja baada ya Mahakama Kuu kuhoji ni kwa nini Waziri Mkuu ameshindwa kuwafungulia mashtaka washtakiwa wa rushwa wakati Katiba ya nchi hiyo inaeleza kinachostahili kufanywa pale kunapokuwa na vitendo vya rushwa.

Mahakama Kuu nchini Pakistan ilitoa  tamko hilo baada ya Jeshi kuiomba  Mahakama kumuagiza Waziri Mkuu Yousuf Raza Gilan kuomba radhi kutokana na kulikosea jeshi kwa kusema limekuwa likiongoza nchi hiyo kwa muda mrefu.
 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.