Pata taarifa kuu
Syria

Watu 34 wauawan baada ya Syria kukubaliana na nchi za kiarabu

Watu thelathini na wanne wameuawa nchini Syria wakati huu ambapo serikali imekubali kwa masharti kuingia waangalizi kutoka Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kuingia katika taifa hilo ikiwa ni sehemu ya kumaliza machafuko yanayoshuhudiwa. Hatua ya Syria kukubali kuwaruhusu waangalizi hao imekuja baada ya Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kuwa tayari kuishushia vikwazo zaidi nchi hiyo inayotajwa kukandamiza haki za waandamanaji. 

REUTERS/Omar Ibrahim
Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa vikwazo vya kibiashara ambavyo vimetangazwa dhidi ya Syria vinaanza kufanyakazi kwani tayari Shirika la Mafuta la Ufaransa, Total limetangaza kusitisha kufanyakazi zake kutekeleza agizo la Umoja wa Ulaya EU.

Awali Syria iliridhia mpango wa jumuiya ya nchi za kiarabu kupeleka waangalizi wa haki za binadamu nchini humo kwa lengo la kumaliza machafuko na ukiukwaji wa haki za binadamu.

Hata hivyo nchi hiyo hapo awali ilikua ikiupinga mpango huo ambao umekua ukishinikizwa na nchi hizo za kiarabu zikiwa na lengo la kukomesha ukiukwaji wa haki za binadamu.

Syria ambayo ilipewa siku moja hadi kufikia jana iwe tayari imesaini makubaliano ya kuruhusu mpango wa jumuiya hiyo kupeleka waangalizi zaidi ya elfu nne kuangalia hali ilivyo nchini humo imesema kuwa ipo tayari kusaini makubaliano hayo endapo mpango huo una lengo la kumaliza machafuko.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Syria Jihad Makdesi amewaambia waandishi wa habari kuwa makubaliano yamefikiwa kwa kuzingatia maslahi ya nchi hiyo na kwamba waziri wa mambo ya nje Walid Muallem tayari amepeleka ujumbe kwenye jumuiya hiyo tayari kwa kutia saini makubaliano hayo.

Mapema mwezi uliopita waziri Muallem alisema kuwa nchi yake haitasaini makubaliano kwa madai kuwa mpango huo ulibe ba ujumbe ambao ulilenga kukandamiza uhuru wa nchi hiyo.

Takribani watu 63 wameuwawa katika machafuko mwishoni mwa juma lililopita, wanaharakati nchini humo wamethibitisha.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.