Pata taarifa kuu
Syria

Syria yakubali nchi za kiarabu kupeleka waangalizi wa haki za binadamu

Syria imeridhia mpango wa jumuiya ya nchi za kiarabu kupeleka waangalizi wa haki za binadamu nchini humo kwa lengo la kumaliza machafuko na ukiukwaji wa haki za binadamu.

Reuters路透社
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo nchi hiyo hapo awali ilikua ikiupinga mpango huo ambao umekua ukishinikizwa na nchi hizo za kiarabu zikiwa na lengo la kukomesha ukiukwaji wa haki za binadamu.

Syria ambayo ilipewa siku moja hadi kufikia jana iwe tayari imesaini makubaliano ya kuruhusu mpango wa jumuiya hiyo kupeleka waangalizi zaidi ya elfu nne kuangalia hali ilivyo nchini humo imesema kuwa ipo tayari kusaini makubaliano hayo endapo mpango huo una lengo la kumaliza machafuko.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Syria Jihad Makdesi amewaambia waandishi wa habari kuwa makubaliano yamefikiwa kwa kuzingatia maslahi ya nchi hiyo na kwamba waziri wa mambo ya nje Walid Muallem tayari amepeleka ujumbe kwenye jumuiya hiyo tayari kwa kutia saini makubaliano hayo.

Mapema mwezi uliopita waziri Muallem alisema kuwa nchi yake haitasaini makubaliano kwa madai kuwa mpango huo ulibe ba ujumbe ambao ulilenga kukandamiza uhuru wa nchi hiyo.

Takribani watu 63 wameuwawa katika machafuko mwishoni mwa juma lililopita, wanaharakati nchini humo wamethibitisha.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.