Pata taarifa kuu
Yemen

Baraza la Usalama la UN kujadili hali ya Yemen

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, Jumatatu juma lijalo, litajadili hatua ya Rais wa Yemen, Ali Abdullah Salleh kukataa kuchia madaraka yake huku kukiwa na ongezeko la machafuko yanayoongeza shinikizo kwa jumuia ya kimataifa la kutaka kiongozi huyo aachie ngazi.

REUTERS/Khaled Abdullah
Matangazo ya kibiashara

Mshindi wa tuzo ya amani la Nobel na mwanaharakati wa nchini Yemen,Tawakul Karman amefanya mazungumzo na ujumbe wa Umoja wa Mataifa hapo jana ikiwa ni sehemu ya kampeni dhidi ya Saleh.

Halikadhalika mwanaharakati huyo hii leo ataongoza mkutano nje ya jengo la umoja wa mataifa, nchini humo kama harakati za kuung'oa utawala wa rais huyo.

Wanachama 15 wa baraza la usalama la umoja wa mataifa kwa pamoja walipitisha azimio namba 2014 tarehe 21 mwezi uliopita wakikemea mashambulizi dhidi ya waandamanaji yanayotekelezwa na vikosi vya serikali ya Yemen.

Aidha Baraza hilo la Usalama limeunga mkono mpango wa Baraza la Jumuia ya nchi za ghuba wa kumshinikiza Saleh kuondoka madarakani baada ya kuliongoza taifa hilo kwa miaka 33.

Mamia ya waandamanaji wameuawa tangu kuanza kwa maandamano nchini humo mwezi januari.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.