Pata taarifa kuu
IRAQ

Shambulio la kujitoa muhanga laua zaidi ya watu 23 nchini Iraq.

Takriban watu ishirini wameuwawa na wengine themanini na watatu wamejeruhiwa katika mfululizo wa mashambulio yaliyotekelezwa katika mji mkuu wa nchi ya Iraq wizara ya ndani ya nchi hiyo imethibitisha.

Mabaki ya gari lililoshambuliwa nchini Iraq.
Mabaki ya gari lililoshambuliwa nchini Iraq. RFI
Matangazo ya kibiashara

Katika moja ya mashambulio,mtu aliyejitoa muhanga ameripotiwa kuendesha gari lililojazwa mabomu katika kituo cha polisi mjini Baghdad na kuua takribani watu sita wakiwemo polisi wanne.

Msemaji wa jeshi la Baghdad Qassim al-Moussawi amelishutumu kundi la Al- Qaeda nchini Iraq kwa kufanya mashambulio hayo na kusema kuwa hayo ni mashambulio ya kujaribu kuwadhihirishia watu kuwa kundi hilo bado lina nguvu na uwezo wa kutishia usalama katika vituo vya usalama.

Mashambulio hayo ya mfululizo ni mabaya kuwahi kutokea mjini Baghdad tangu kutokea shambulio katika msikiti mkuu wa madhehebu ya Sunni na kuua watu ishirini na nane mwishoni mwa mwezi August,shambulio linalodaiwa kutekelezwa na kundi la Al- Qaeda
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.