Pata taarifa kuu
Yemen

Rais Saleh wa Yemen aibuka na vikwazo vipya

Rais wa Yemen Ali Abdullah Saleh ameibuka na vikwazo vingine ili aweze kukaa kando kwa kusema ataendelea kutawala nchi hiyo iwapo washirika wake wa zamani ambao kwa sasa wamegeuka wapinzani wataruhusiwa kushiriki uchaguzi mkuu.

REUTERS/Mohamed al-Sayaghi
Matangazo ya kibiashara

Rais Saleh ambaye baada ya kurejea nyumbani kutoka nchini Saudi Arabia alikokuwa anapatiwa matibabu aliahidi kuachia madaraka na kuitisha uchaguzi mapema sasa amekuwa kigeugeu na kusema hatofanya hivyo iwapo wshirika wake wa zamani watagombea.

Rais Saleh amejiapiza hawezi kukubali kuona washirika wake hao wa zamani wanawania uraisi kwa hofu huenda wakafanya mapinduzi iwapo watashindwa kwenye kisanduku cha kupigia kura.

Kiongozi huyo ambaye anakumbana na upinzani mkubwa wa kumtaka aondoke madarakani ameongeza kuwa hofu kubwa ambayo anayo yeye ni huenda nchi hiyo ikaingia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe iwapo watu hao watachukua madaraka.

Rais Saleh anasema ni wazi washirika wake hao wa zamani ambao kwa sasa ni wapinzani watahitaji kulipiza kisasi kwa wale ambao hawawaungi mkono hatua ambayo itakuwa ni hatari kubwa kwa Taifa.

Rais Saleh ambaye amekuwa king'ang'anizi wa madaraka mara kadhaa amekuwa akitoa ahadi ambazo hazitekelezeki na kuchangia hasira kwa wapinzani nchi humo ambao wamekuwa wakifanya maandamano kila kukicha.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.