Pata taarifa kuu
SYRIA

Watu 15 wapoteza maisha nchini Syria wakati Mkuu wa ICRC akizuru Taifa hilo

Watu kumi na tano wamepoteza maisha nchini Syria wakati nchi hiyo ikiendelea kushuhudia machafuko yakizidi kushika kasi kipindi hiki ambacho wanaharakati wapo mstari wa mbele kutaka mabadiliko ya utawala.

REUTERS/Murad Sezer
Matangazo ya kibiashara

Habari ambazo zimetolewa na Kituo cha Habari za serikali cha SANA zimeeleza kuwa wanajeshi sitau wamepoteza maisha na raia watatu baada ya kundi la watu wenye silaha kushambulia basi la abiria katika eneo la Maharda.

Taarifa zinaweka bayana katika shambulizi hilo lililogharimu maisha ya ya watu tisa na kujeruhi kumi na saba limetokea wakati basi lililokuwa limewabeba wanajeshi na wafanyakazi likikatiza katika eneo la Maharda.

Habari zaidi zinasema kuwa baada ya kutokea kwa shambulizi hilo wanajeshi wakalazimika kujibu mashambulia ambapo walifanikiwa kuwaua watu watatu na wengine wanne wakajeruhiwa.

Ulinzi umeimarishwa katika Hospital ambayo wamehifadhiwa majeruhi hao kwa kile ambacho polisi wanasema wanahofi ya kutoroshwa kwa majeruhi hao na kwenda kutibiwa sehemu nyingine.

Nchi ya Syria inayoshuhudia machafuko yaliyodumu kwa miezi mitano sasa imekuwa katika kipindi kigumu kutokana na wanaharakati kutaka utawala wa Rais Bashar Al Assad uondoke madarakani.

Hapo jana Mkuu wa Shirika la Msalaba Mwekundu Duniani ICRC Jakob Kellenberger ameelekea Mji Mkuu wa Syria, Damscus kufanya mazungumzo na Rais Assad ili waweze kupata nafasi ya kuwahudumia wafungwa pamoja na kufika kwenye maeneo yenye machafuko.

Mapigano haya mapya yamekuja wakati ambapo Mawiziri kutoka Nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya EU wakitoa onyo la kuweka vikwazo zaidi kwa taifa la Syria ikiwa ni njia la kutaka kusitishwa kwa mauaji.

Hadi sasa takwimu za Umoja wa Mataifa UN zinaonesha kuwa watu zaidi ya 2200 wameshapoteza maisha katika kipindi cha miezi mitano ya machafuko ambayo yameshuhudia katika nchi ya Syria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.