Pata taarifa kuu
LEBANON

Mahakama ya Umoja wa Mataifa UN yatoa hati ya kukamatwa kwa maofisa 4 wa Hezbollah

Mahakama ya Umoja wa Mataifa imetoa hati ya kukamatwa kwa viongozi wanne wa chama cha Hezbollah ambao wametajwa kuhusika na mauaji ya waziri mkuu wa zamani wa Lebanon Rafik al-Hariri mwaka 2005.

Sehemu ya kaburi alikozikwa waziri mkuu wa zamani wa Lebanon Rafiki al-Hariri
Sehemu ya kaburi alikozikwa waziri mkuu wa zamani wa Lebanon Rafiki al-Hariri REUTERS/ Jamal Saidi
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa taarifa kutoka nchini Lebanon zinasema kuwa mwendesha mashtaka mkuu wa nchi hiyo Saeed Mirza amepokea barua rasmi toka kwa majaji wa mahakama hiyo kumtaka kuwafikisha watu hao wanne waliotajwa mbele ya mahakama.

Katika barua hiyo imewataja viongozi hao wanne wa Hezbollah ambao ni Mustafa Badreddine, Salim al-Ayyash, Hassan Issa na Asad Sabra ambpo mwendesha mashtaka huyo amepewa siku 30 kupitia ushahidi kabla ya kuwafikisha mbele ya mahakama viongozi hao.

Tangu kuanza kwa upelelezi wa tukio la kuuawa kwa waziri mkuu Hariri, viongozi wa chama cha Hezbollah wamekuwa wakikanusha kuhusika na njama zozote za kupanga mauaji ya waziri mkuu huyo wa zamani.

Tayari mtoto wa Hariri, Saad Hariri ambaye nae alikuwa waziri mkuu kabla ya kung'atuka madarakani, amepokea taarifa hizo na kudai kuwa kama zinaukweli wowote basi itakuwa ndio mwanzo kupatikana kwa watu waliohusika na mauaji ya baba yake.

Wachambuzi wa masuala ya siasa nchini humo wanasema kuwa hata kama majina hayo yatakuwa yametolewa basi huenda viongozi hao wasikamatwe na kufikishwa mbele ya mahakama hiyo kwa kile kilichoelezwa ni kutokana na serikali ya sasa kuongozwa na chama hicho.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.