Pata taarifa kuu
PAKISTAN

Pakistan yawafukuza maofisa mafunzo 20 wa jeshi la Uingereza

Wizara ya mambo ya ndani ya Pakistan imetangaza kuwaondoa maofisa wa jeshi la Uingereza ambao wamekuwa wakishiriki katika kutoa mafunzo kwa wanajeshi wa Pakistan walioko mstari wa mbele kupambana na wapiganaji wa kundi la Al-Qaeda.

Askari wa Marekani akiwa katika doria nchini Pakistan
Askari wa Marekani akiwa katika doria nchini Pakistan REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Kuondolewa kwa maofisa hao zaidi ya 20 wa jeshi la Uingereza kumekuja kufuatia ombi la serikali ya Pakistan kuitaka nchi hiyo kuwaondoa maofisa wake wa mafunzo kwa kile walichoeleza ni sababu za kiusalama.

Msemaji wa jeshi la Pakistan amesema kuwa kuondolewa kwa maofisa hao wa mafunzo wa Uingereza hakumanishi kuvunja uhusiano baina ya nchi hizo mbili kiusalama bali hatua hiyo ni ya muda na usalama ukirejea maofisa hao watarejeshwa.

Tangu kufanyika kwa operesheni ya kijeshi na makomandoo wa Mareakani nchini humo na kufanikiwa kumuua kiongozi wa mtandao wa kigaidi duniani wa Al-Qaeda, Osama Bin Laden, serikali ya Pakistan imekuwa ikivituhumu vikosi vya Marekani na Uingereza kufanya baadhi ya mashambulizi bila kushirikisha jeshi la Pakistan.

Tayari majeshi ya Marekani yametangaza kuondoa maofisa wake wa mafunzo zaidi ya 100 toka nchini Pakistan ikiwa ni sehemu ya ombi la wizara ya mambo ya ndani ya Pakistan kutaka maofisa hao kuondolewa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.