Pata taarifa kuu
PAKISTAN-WAZIRISTAN

Wanajeshi 8 wa Pakistan wauawa katika jimbo la Waziristan na wanamgambo wa Taliban

Wanajeshi sita wa Pakistan wameuawa wakati wakiwa katika kituo kimoja cha ukaguzi kusini mwa jimbo la waziristan lililoko mpakani mwa nchi hiyo na Afghanistan baada ya wanamgambo wa Taliban zaidi ya 100 kuwahsmabulia kituo hicho kwa roketi.

Ramani inayoonyesha eneo la Waziristan Kaskazin
Ramani inayoonyesha eneo la Waziristan Kaskazin
Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo linakuwa ni la pili kufanywa na wapiganaji wa Taliban ndani ya Juma moja katika vituo vya ukaguzi vya wanajeshi wa Pakistan katika jimbo la waziristan na kuendelea kuzua hofu kwa wananchi wa eneo hilo.

Msemaji wa polisi katika jimbo hilo amesema kuwa wanajeshi nane wa Pakistan wameuawa na wanajeshi kumi wa Taliban wamedhibitishwa kufa katika majibizano ya risasi.

Shambulio hilo limefanyika hii leo katika eneo la mpaka wa nchi hiyo na Afghanistan aneo ambalo vikosi vya Marekani vimepiga kambi kitendo kinachoelezewa kuwa wanamgambo hao walilenga kushambulia kambi hiyo.

Serikali ya Marekani imelitaja eneo la Waziristan lililoko kaskazini mwa Pakistan kuwa ni eneo hatari zaidi duniani ambalo ndio makao makuu ya kundi la Taliban na Al-Qaeda ambao wamekuwa wakiendesha mashambulizi dhidi ya vikosi vya Pakistan.

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Hillary Clinton tayari ameitaka serikali ya Pakistan kuanzisha operesheni maalumu ya kijeshi katika eneo hilo kuwasaka wanamgambo wa Taliban ambao wamekuwa wakitokea milimani na kufanya mashambulizi ya kushtukiza.

Mwaka 2009 majeshi ya Marekani kwa kushirikiana na vikosi vya Pakistan vilifanya operesheni maalumu katika eneo hilo na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kuisambaratisha ngome ya wapiganaji wa Taliban ambao sasa wamerejea tena na kujiimarisha.

Wachambuzi wa masuala ya usalama wameendelea kuhoji uimara wa usalama wa taifa wa Pakistan ambao mara kadhaa imeshuhudiwa wakizidiwa nguvu na wapiganaji wa Taliban.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.