Pata taarifa kuu
Yemen

Majeshi ya Yemen yaua waandamanaji 20

Vikosi vinavyomtii rais wa Yemen Ali Abdullah Salleh vimewaua waandamanaji 20 wakati walipofanya maandamano mjini Taez, waratibu wa maandamano hayo wamethibitisha.

Mmoja wa waandamanaji jijini Taiz, Yemen akizuiwa na askari wa kutuliza ghasia.
Mmoja wa waandamanaji jijini Taiz, Yemen akizuiwa na askari wa kutuliza ghasia. REUTERS/Khaled Abdullah
Matangazo ya kibiashara

Duru za hospitali zimesema huenda idadi hiyo ikaongezeka, na kwamba mamia wamejeruhiwa.
Hapo jana, polisi walifyatua risasi za hewa ya kutoa machozi na mabomba ya maji kuwatawanya waandamanaji nje yajengo la halmashauri ya jiji. Waandamanaji hao walikuwa wakidai mwenzao mmoja aliyekamatwa aachiliwe huru.
Takriban watu 37 waliokuwa wakipata huduma hospitalini, wanashikiliwa na vikosi vya usalama nchini humo
Wapinzani nchini humo wamelaani vitendo hivyo na kumuonya Salleh kuwa atawajibika kwa vitendo vya kinyama anavyoviendeleza dhidi ya raia wake.
Mapigano hayo yameibuka jana jioni, nje ya kituo cha polisi wakati takriban watu 3000 walipojitokeza kudai kuachiwa kwa mwenzao aliyekuwa akishikiliwa na polisi.
Zaidi ya waandamanaji 200 wameuawa tangu maandamano yalipozuka kwa mara ya kwanza nchini humo, baada ya kuzuka kwa mapigano kati ya raia na vikosi vya Rais Ali Abdullah Saleh.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.