Pata taarifa kuu
YEMEN

Marekani yaagiza wanadiplomasia wake waondoke Yemen

Marekani imewaagiza wanadiplomasia wanaofanya kazi katika ubalozi wake nchini Yemen pamoja na familia zao kuondoka mara moja baada ya mapigano makali kuzuka nchini humo.

REUTERS/Khaled Abdullah
Matangazo ya kibiashara

Aidha Serikali ya Marekani imewazuia raia wake kusafiri kwenda nchini Yemen kwa kuhofia usalama wa nchi hiyo ambayo inakabiliwa na machafuko makubwa ya kisiasa.

Mapigano hayo yanatokea huku rais wa nchi ya Yemen, Ali Abdullah Saleh kuapa kuondoka Yemen hata kama maandamano ya kumpinga na kutaka aondoke madarakani yataendelea.

Rais huyo amekataa kusaini makubaliano ya mpango wa mpito wa kuleta mabadiliko ya kisiasa ambayo yangemlazimu kujiuzulu na hatimaye kuruhusu kuundwa kwa Seriakali ya umoja wa kitaifa.

Watu wasiopungua 44 wameuawa tangu kuanza upya kwa mapambano yaliyozuka jumatatu wiki hii baina ya wapiganaji wa kikabila na wanajeshi wa Serikali ya Yemen.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.