Pata taarifa kuu
PAKISTAN

Watu 16 wamekufa katika shambulio la bomu nchini Pakistan

Watu 16 wamekufa na wengine kadhaa wamejeruhiwa kaskazini mashariki mwa nchi ya Pakistan kufuatia shambulio la bomu kwenye gari la mafuta lililokuwa likipelekea mafuta hayo katika kambi za majeshi ya NATO yaliyoko Afghanistan.

Moja ya gari la mafuta la NATO likiwaka moto baada ya kushambuliwa nchini Pakistan
Moja ya gari la mafuta la NATO likiwaka moto baada ya kushambuliwa nchini Pakistan Reuters
Matangazo ya kibiashara

Tukio hili ni mfululizo wa matukio kama haya yaliyotekelezwa ndani ya wiki mbili na wafuasi wa kundi la wanamgambo wa Talibani kwa kile kinachoonekana ni ulipizaji kisasi kutokana na kifo cha kiongozi wa kundi la Al Qaeda Osama Bin Laden aliyeuawa na majeshi ya Marekani.

Polisi katika mji wa Torkham mpakani na nchi ya Afghanistan wamesema kuwa shambulio la kwanza lililenga gari hilo la mafuta ambapo wakati watu wamekusanyika kushuhudia mlipuko huo ghafla kukatokea mlipuko wa pili katika gari hilohilo asubuhi ya hii leo na kuua watu hao 16.

Msemaji wa kundi la Taliban Pakistan, Abdullah Azzam Brigade, amekiri kundi lake kuhusika na sambulio hilo ambapo pia siku ya ijumaa kundi lake lilishambulia msafara wa magari kumi na sita ya mafuta yaliyokuwa tayari kupeleka mafuta katika vikosi vya majeshi ya NATO na yale ya Marekani yaliyoko nchini Afghanistan ingawa katika shambulio la ijumaa hakukuwa na mtu aliyejeruhiwa.

Kundi hilo limeapa kuendeleza mashambulizi dhidi ya vikosi vya Pakistan na washirika wake likisema kuwa ni kulipiza kisasi kwa kile ambacho makomandoo wa Marekani walikifanya majuma kadhaa yaliyopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.