Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho
Siku ya kimataifa ya kuadhimisha hewa safi duniani yaadhimishwa
Imechapishwa:
Cheza - 09:06
Mnamo Septemba 7, dunia iliadhimisha siku ya hewa safi duniani, maadhimisho ambayo yalifanyika katika kipindi ambacho dunia bado inakabiliwa na tishio la hali ya mabadiliko ya tabianchi kuzidi kuwa mbaya zaidi.Uchafuzi wa hewa umesababisha ongezeko la joto duniani, hali hii ikichangia majanga kama viale moto wa nyika.Katika makala yetu juma hili, tutakuwa tukiangazia swala la uchafuzi wa hewa, pamoja na hatua zinazochukuliwa na washikadau katika sekta ya mazingira kuangazia hili tatizo hili.