Pata taarifa kuu
Habari RFI-Ki

Je viongozi wa Africa wanaweza kufikishwa mahakamani

Imechapishwa:

Rais wa zamani wa Marekani afikishwa mahakamani na kufunguliwa mashtaka 34 ya uhalifu dhidi yake, mashtaka ambayo Donald Trump amekana yote.

USA-TRUMP/
USA-TRUMP/ REUTERS - BRENDAN MCDERMID
Matangazo ya kibiashara

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump, 76, mgombea wa uchaguzi wa urais wa mwka 2024, anapitia wakati wa kihistoria wa kimahakama Jumanne, Aprili 4, alipofikishwa katika mahakama ya jinai kusomewa mashtaka yake, katika kesi ya ulaghai inayohusishwa na pesa zilizolipwa kwa mwingizaji wa filamu za watu wazima mwaka 2016.

Donald Trump hana hatia. Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump ametupilia mbali mashtaka dhidi yake katika kesi ya kihistoria ya uhalifu katika mahakama ya New York.

Bw. Trump anashtakiwa kwa kosa la unyanyasaji kuhusiana na pesa zilizolipwa kwa mwingizaji wa filamu za watu wazima mwaka 2016. Ilibidi ashtakiwe katika kesi ambayo itakuwa na uzito mkubwa katika azma yake ya kushinda uchaguzi wa urais.

Nchini mwako kiongozi wa ngazi ya juu, anaweza fikishwa mahakamani ndilo swali tumekuuliza.

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump akiwa Palm Beach, Florida, Marekani, Aprili 4, 2023.
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump akiwa Palm Beach, Florida, Marekani, Aprili 4, 2023. © REUTERS / MARCO BELLO
Vipindi vingine
  • 10:00
  • 10:13
  • 10:00
  • 09:51
  • 09:52
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.