Msikilizaji wakati mkutano wa kimataifa wa Jukwaa la Uchumi duniani World Economic Forum, ukiendelea kwenye mji wa Davos, Uswis, shirika la kimataifa linalopambana na umasikini, Oxfam, linasema kwenye ripoti yake kuwa, tunaishi katika nyakati ngumu zenye kushuhudia mizozo tofauti, mamia ya watu wanakabiliwa na njaa, kupanda kwa gharama za maisha, na kwamba umasikini umasikini umeongezeka kwa kiwango cha juu katika kipindi cha miaka 25.
Vipindi vingine
-
Afrika na madai ya mabadiliko katika mifumo ya kifedha ya kimataifa
Msikilizaji katika miaka ya hivi karibuni, wito umeendelea kutolewa na mataifa ya Afrika kuhusu kuwepo usawa na haki katika mfumo wa kifedha duniani, ambao Kihistoria, nchi za Kiafrika zimekuwa katika hali mbaya linapokuja suala la kupata ufadhili, rasilimali, na makubaliano yenye usawa ya kibiashara.Kuzungumzia hili, nimemualika kwa njia ya simu kutoka Tanzania, Walter Nguma, mtaalamu na mchambuzi wa masuala ya uchumi na biashara.01/05/202409:40 -
Wataalamu: Uchumi Samawati utumiwe vizuri kwa maendeleo endelevu
Kulingana na Benki ya Maendeleo ya Afrika, uchumi wa bluu barani Afrika una uwezo wa kuchangia pakubwa katika ukuaji wa uchumi na maendeleo ya bara hilo.Uchumi wa bluu unatajwa kuchangia dola za Marekani trilioni 1 kila mwaka, Sekta ya uvuvi ikiwa kitovu kikuu na kuajiri zaidi ya watu milioni 12.Profesa Omary Mbura, mtaalamu na mhadhiri wa masuala ya uchumi kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam, anaangazia sekta hii.11/04/202410:02 -
Umuhimu wa ushirikiano kati ya sekta binafsi na uma
Shughuli za sekta binafsi na uwekezaji ni vyanzo vikuu ya ukuaji wa uchumi, uzalishaji wa ajira na maendeleo endelevu.Kwa wastani, sekta binafsi inachangia zaidi ya Asilimia 80 ya mapato ya serikali kwa watu wa kipato cha chini na cha kati, kupitia kodi ya kampuni, kodi ya rasilimali na mapato ya kodi kwa wafanyakazi.Sekta hii inazalisha zaidi ya asilimia 90 ya ajira katika nchi zinazoendelea kiuchumi.04/03/202410:00 -
Ukulima wa matunda Kenya na changamoto zake
Makala ya Gurudumu la Uchumi, juma hili inaangazia kilimo cha matunda nchini Kenya, na namna wakulima wa nchi hiyo, wameendelea kukumbatia mbinu mpya za kilimo, uvunaji na usindikaji.04/03/202410:00 -
Changamoto za uhamiaji na fursa zake kwa uchumi
Uhamiaji unaweza kuwa nguzo muhimu kwa maendeleo ya uchumi wa Afrika ikiwa mtu anaweza kutoa mwelekeo bora wa fedha zinazotumwa na wageni kuelekea uwekezaji na ufadhili wa maendeleo katika nchi za Afrika.Diasporas wanachangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya nchi zetu ambazo kimsingi ni nchi za asili lakini pia nchi mwenyeji.04/03/202410:04