Pata taarifa kuu
Marekani- Israeli- Diplomasia

Rais wa Marekani Barck Obama amtaka Benjamin Netanyahu waziri mkuu wa Israeli kufanya maamuzi magumu ili kufikia amani na jirani zake wa Palestina

Waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahju ameanza ziara jana nchini Marekani ambapo amaejadiliana na rais Barack Obama juu ya mchakato wa amani kati ya Israeli na palestina pamoja na mpango wa nyuklia wa Iran. Benjamin Netanyahu anaonakuwa mkataba uliofikiwa juu ya swala la nyuklia ya Iran, ni kosa kubwa la kihistoria. Upande wake Rais wa Marekani Barack Obama amemwambia Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kuwa ni lazima afanye uamuzi mgumu ili kufanikisha mazungumzo ya amani kati yake na Palestina.

Rais Obama wa marekani na waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu
Rais Obama wa marekani na waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu
Matangazo ya kibiashara

Obama amekutana na Netanyahu katika Ikulu ya Marekani jijini washington DC na kusisitiza kuwa bado ana matumaini ya mwafaka kufikiwa kufikia tarehe 29 mwezi wa nne. Netanyahu naye amemtaka rais Barrack Obama kusimama na watu wa Isreal katika harakati hizi na kuishawishi Palestina kutekeleza jukumu lao ili mwafaka ufikiwe kwa haraka.

Barack Obama na Benjamin Netanyahu hawaelewani. Viongozi hawa wawili walichukuwa uongozi mwaka mmoja wa 2009, na tangu hapo kumetokea mara kadhaa hali ya tahadhari hususan kila wakati rais Obama anapo jaribu kumtaka Benjamin Netanyahu kuweka kando baadhi ya mambo ili mchakato wa mazungumzo na wapalestina ufikie hatuwa.

Wataalamu wa maswala ya Diplomasia wanaokuwa uhusiano wa Benjamin Netanyahu na rais kutoka chama cha Demokrate, hauendi sawa licha ya kushuhudia ziara ya viongozi wa mataifa hayo mara kadhaa hususun ziara ya rais Obama mwaka uliopita nchini Israeli, na sasa wamekuwa wakikutana kujaribu kumaliza tofauti zao.

Wakati Benjamin Netanyahu akikutana na Rais  Obama, Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas naye anatarajia kuzuru Marekani kushauriana na rais Obama juu ya mchakato wa amani kati ya Israeli na Palestina.

Kuhusu swala la Nyuklia ya Iran, waziri mkuu wa Israeli anaonakuwa hautwa iliofikiwa ya kulegeza vikwazo dhidi ya Iran, haikupashwa kufikia, kwakuwa kitisho cha iran kumiliki bomu ya Atomiki ni kikubwa mno kwa Israeli.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.