Pata taarifa kuu
URUSI-KIFO CHA ARAFAT

Ripoti ya wataalamu wa Urusi kuhusu kifo cha rais wa zamani wa Mamlaka ya wa Palestina yabaini kuwa hakuna ushahidi wa kuuawa kwa sumu

Wataalamu wa Urusi wanaofanya uchunhuzi juu ya kiini cha kifo cha aliyekuwa rais wa mamlaka ya wa Palestina Yasser Arafat wamesema kuwa kiongozi huyo aliuawa kufuatia kifo cha kawaida na sio simu kama ilivyo fahamishwa.

Rais wa mamlaka ya wa Palestina  Yasser Arafat zama za uhaiwake May 5, 2001
Rais wa mamlaka ya wa Palestina Yasser Arafat zama za uhaiwake May 5, 2001 REUTERS/Suhaib Salem/Files
Matangazo ya kibiashara

Vladimir Ouiba, mkurugenzi wa kituo cha uchunguzi wa kibaiologia amesema kiongozi huyo alipoteza maisha kutoka na maradhi ya kawaida, na hivo kuungana na upande wa pili wa ripoti kama hiyo iliotolewa na wataalamu wa Ufaransa ambao nao pia walibaini kuwa hapakuwa na ushahidi wa kutosha juu ya kifo cha kiongozi huyo kuhusika na sumu. Ripoti hiyo ya wataalamu wa Ufaransa ilitupiliwa mbali na mjane wa Arafat, Suhat Arafat.

Balozi wa Palestine nchini Urusi Faed Mustafa amesema uchunnguzi bado unaendelea kubaini chanzo cha kifo cha kiongozi wa kihistoria wa Mamlaka ya wa Palestina Yasser Arafat aliye uawa mwaka 2004 akiwa na umri wa miaka 75
katika Hospitasli ya Percy, karibu na Paris.

Viongozi wa Palestina wanaituhumu Israeli kuhusika na kifo cha kiongozi wao na kuomba uundwaji wa tume ya kimataifa ya uchunguzi juu ya tuhuma hizo.
Ma jaji nchini Ufaransa waliamuru kuuzua mwili wa kiongozi huyo mwezi Novemba mwaka 2012, na viashiria zaidi ya sitini vilichukuliwa na kupewa timu tatu tofauti za wataalumu kutoka Urusi, Ufaransa na Uswisi.

Mahakama ya Nante karibu na jiji la Paris ilitowa ripoti ya watalaam waliosema hapakuwa na sumu yoyote ya polonium, ripoti ambayo ilitupiliwa mbali na mjane wa Arafat Souhat Arafat ambaye alisema ataipinga ripoti hiyo mahakamani.

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.