Pata taarifa kuu
ISRAEL-PALESTINA-MAREKANI

Ujumbe wa Palestina kwenye mazungumzo ya amani na Israel watangaza kujiuzulu, Abbas asema hakuna mjadala

Timu ya wapatanishi wa Palestina kwenye mzozo wa nchi yao na Israel wametangaza kujiuzulu nafasi zao kwakile wanachodai ni kuendelezwa kwa makazi ya kudumu na Serikali ya Israel kwenye eneo lenye mzozo na pia kushindwa kwa juhudi za Marekani kwenye kupata suluhu. 

Waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu akiwa na mwenzake rais wa mamlaka ya Palestina, Mahamoud Abbas
Waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu akiwa na mwenzake rais wa mamlaka ya Palestina, Mahamoud Abbas Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa ujumbe wa wapatanishi wa Palestina, Mohamed Shtayyeh amethibitisha ujumbe wake wote kuandika barua kwa rais wa mamlaka ya Palestina Mahamoud Abbasi kumueleza nia yao ya kujiuzulu kwenye nafasi zao.

Shtayyeh kwenye barua yake kwa rais Abbasi wamemweleza kutoridhishwa kwao na hatua ambazo zinachukuliwa na nchi ya Marekani katika kupata suluhu ya neoe la ukanda wa Gaza na Jerusalem ambako nchi ya Israel imeendelea na ujenzi wa makazi ya kudumu.

Juma hili Serikali ya Israel ilitangaza kusitisha kwa muda ujenzi kwenye baadhi ya maeneo lakini ikaendelea na ujenzi kwenye maeneo yenye mzozo kati yake na Palestina jambo ambalo limeamsha hasira kwa ujumbe huo.

Hata hivyo rais Abbas bado hajajibu barua za wajumbe wake kujiuzulu nafasi zao ingawa kuna uwezekano mkubwa akakubaliana na maamuzi ya wapatanishi wake kwakuwa hata yeye emchukizwa na hatua ya Israel.

Kujiuzulu kwa wapatanishi hawa kunakuja ikiwa zimepita saa chache toka mamlaka ya Palestina itoe tangazo la kujiondoa kwenye mazungumzo ya amani kati yake na Israel kufuatia hatua ya nchi hiyo kuendeleza makazi zaidi.

Mamlaka ya Palestina inaituhumu nchi ya Marekani kwakuwa sehemu ya mgogoro huo licha ya kufanya juhudi za kujaribu kuwapatanisha lakini imekuwa ikiitetea Serikali ya Israel kutokana na ushirikiano iliyonayo.

Wachambuzi wa mambo wanaona kuwa kujiuzulu kwa wapatanishi wa Palestina kwenye mzozo wao na Israel ni pigo kuelekea kupata amani ya kudumu kati ya nchi hizo mbili kwakuwa sasa watarejea kwenye mapigano ya kugombania maeneo ya walowezi wa Israel na Palestina.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.