Pata taarifa kuu
DRC-M23-UGANDA

Kundi la waasi wa M23 lagawanyika kuhusu kutia saini mkataba wa amani na Serikali ya DRC

Kundi la waasi wa M23 la nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo limeelezwa kugawanyika kuhusu utiwaji saini mkataba wa amani kati yake na Serikali ya Kinshasa, hatua inayokuja ikiwa imepita siku kadhaa toka mazungumzo ya kampala yavunjike.Taarifa kutoka mjini Kampala zinasema kuwa kuna kundi jingine ambalo limejitenga kutoka kundi la waasi wa M23 ambalo lenyewe linaunga mkono mapendekezo yaliyokuwa yametangazwa na Serikali.

Ujumbe wa waasi wa M23 ambao ulikuwa mjini Kampala juma hili ukiongozwa na Rene Abandi
Ujumbe wa waasi wa M23 ambao ulikuwa mjini Kampala juma hili ukiongozwa na Rene Abandi REUTERS/James Akena
Matangazo ya kibiashara

Mgawanyiko huu unakuja ikiwa ni juma hili tu toka waasi hao washindwe kutiliana saini mkataba wa amani kati yake na Serikali ya Kinshasa ambayo imesisitiza kutotia saini mkataba wa amani na badala yake itatia saini azimio la amani.

Taarifa iliyotolewa na kundi lililojitenga na rfikiswahili kupata nakala yake, inasema kuwa wao hawaungi mkono madai ya wenzao na badala yake wanataka kukubaliana na Serikali ya DRC kuhusu kutia saini azimio la amani kwa mustakabali wa wananchi wa Kongo.

Taarifa hiyo iliyotiwa saini na Serge Kambasu Ngeve anayedai ni katibu mkuu wa kundi lililojitenga, inasema kuwa wao wako tayari kuzungumza na Serikali ya Kinshasa katika kutafuta njia muafaka za wao kusalimisha silaha na kutia saini azimio la amani.

Rfikiswahili iliwatafuta viongozi wa juu wa kundi la M23 lakini hawakuweza kupatikana kwa wakati ili kuzungumzia suala la kuwepo mgawanyiko ndani ya kundi hilo ingawa taarifa za siri pia zinaeleza baadhi ya viongozi hao wanatofautiana kuhusu suala la amani mashariki mwa nchi hiyo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.