Pata taarifa kuu
SOMALIA-AMISOM-HRW

HRW: Yataka uchunguzi mpya dhidi ya wanajeshi wa AU wanaotuhumiwa kubaka nchni Somalia

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Human Right Watch hii leo limetoa wito kwa Serikali ya Somalia kuanzisha uchunguzi mpya na wa wazi kuhusu tuhuma za ubakaji zinazowakabili wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika nchini humo.

Baadhi ya wanajeshi wa kikosi cha Uganda wanaounda jeshi la AMISOM nchini Somalia
Baadhi ya wanajeshi wa kikosi cha Uganda wanaounda jeshi la AMISOM nchini Somalia Reuters
Matangazo ya kibiashara

Shirika hilo kwenye taarifa yake linasema kuwa muitikio wa Serikali ya Somalia kwenye tuhuma za ubakaji zinazowakabili wanajeshi wa Umoja wa Afrika nchini humo umekuwa mdogo toka tukio hilo liripotiwe mwezi August mwaka huu.

Taarifa hiyo imeeleza kwa kina namna ambavyo zoezi la uchunguzi limefanyika huku kukiwa na mizengwe mingi ya kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa huku baadhi ya wanawake wakitishiwa maisha yao iwapo watasema ukweli.

Mwezi August mwaka huu, mwanamke mmoja aliripoti kubakwa na wanajeshi wa Umoja wa Afrika baada ya kudai kuwa alikamatwa na polisi mjini Mogadishi na kisha kuwekwa kwenye gari kabla ya kupelekwa kwenye kambi moja ya wanajeshi wa AU na kumbaka.

Shirika hilo linataka kufanyika upya kwa uchunguzi wa tukio hilo likidai kuwa baadhi ya viongozi wa Serikali na hata viongozi wa kijeshi wa vikosi vya AMOSOM wamekuwa wakishiriki njama za kutaka kukwamisha uchunguzi huo.

Shirika hilo limeongeza kuwa ni miezi mitatu sasa toka kuripotiwa kwa tukio hilo na kuanza kwa uchunguzi lakini mpaka sasa hakuna fedha zozote zilizotangazwa kutolewa kuwezesha uchunguzi huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.