Pata taarifa kuu
KENYA-ICC-RUTO-SAN'G

Kesi dhidi ya naibu wa rais wa Kenya kwenye mahakama ya ICC, yaingia siku yake ya pili hii leo

Kesi ya uhalifu dhidi ya binadamu inayomkabili naibu wa rais wa Kenya, William Ruto na mwandishi wa habari Joshua Arap San'g imeingia siku yake ya pili hii leo mjini The Hague kwenye makao makuu ya mahakama ya ICC.

Naibu wa rais wa Kenya, William Ruto akiwa kwenye mahakama ya ICC kujibu mashtaka ya uhalifu wa kibanadamu inayomkabili
Naibu wa rais wa Kenya, William Ruto akiwa kwenye mahakama ya ICC kujibu mashtaka ya uhalifu wa kibanadamu inayomkabili Reuters
Matangazo ya kibiashara

Hapo jana William Ruto na Arap San'g walikana mashtaka yanayowakabili mebele ya jopo la majaji watatu wanaosikiliza kesi hiyo huku mawakili wao wakisistiza kuwa wateja wao hawana hatia.

Wakili wa Ruto, Karim Khan amesema mteja wake hana hatia khusu makosa yanayomkabili kwenye mahakama hiyo na kwamba ofisi ya mwendesha mashtaka imefanya makosa makubwa sana kumshtaki mtu ambaye hakuhusika na vurugu za mara baada ya uchaguzi mkuu.

Wakili Khan ameituhumu ofisi ya mwendesha mashtaka wa ICC kwa kushindwa kufanya uchunguzi wa kutosha kuhusu kesi hizo na kwamba walikurupuka na kinachofanyika sasa ni kumkomoa mteja wake.

Wakili hiyo ameongeza kuwa ataendelea kuwathibitishia majaji wa mahakama hiyo kuwa mteja wake hana hatia na kesi hizo zilifunguliwa mahsusi zikiwalenga watu wachache akiwemo William Ruto na Uhuru Kenyatta.

Hata hivyo mwendesha mashtaka Fatou Bensouda amesisitiza kuwa ofisi yake itathibitisha bila shaka kuwa watuhumiwa wote watatu wamehusika na machafuko ya mara baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007-2008.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.